Zari ashangazwa na taarifa za kuachana na Diamond

Mama wa watoto wa Mwanamuziki wa bongo fleva, Diamond Platinumz, Zari Hassan amekanusha kuhusu kuachana na mpenzi wake huyo na kusema, kuwa anashangazwa na uvumi huo ulipotokea.

Zari ambaye yuko nchini, kwaajili ya uzinduzi wa kuwa balozi wa duka la samani la Danube, amesema, yeye na mpenzi wake huyo wameamua kutoweka tena mapenzi yao hadharani na huku wakiendelea kushauriana namna ya kumaliza tofauti zilizojitokeza.

Akifafanua kuhusu, kuondoa picha zote za Diamond katika mitandao ya kijamii, sanjari na kutohudhuria sherehe za kuzaliwa kwa baba watoto wake, amesema, ni uamuzi ambao walikubaliana kwa pamoja.

Sintofahamu ya wawili hao ilitokea hivi karibuni baada ya Diamond kukiri kuzaa na mwanamke wa nje, Hamisa Mobeto kulikoamsha taharuki katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mbalimbali huku kukiwa na taarifa mchanganyiko kuhusu hatima ya wawili hao.

Alisema: “Nilimtakia siku njema ya kuzaliwa lakini sio hadharani bali katika mtandao wa Whatsup. Tunajaribu kuondoa maisha yetu kibinafsi katika mitandao ya kijamii. Na kila tunapoendelea kujiondoa katika mitandao ya kijamii ndiyo tunazidi kupata uvumi, lakini hakuna tatizo kama hilo kila kitu kiko shwari, Zari alisema katika mahojiano na idhaa moja maarufu ya Tanzania.”

Habari za penzi lao kuisha zilizusha madai kwamba hatua hiyo itaathiri mikataba ya mamilioni ya fedha waliotia saini ikiwemo kampuni kadhaa.

Facebook Comments