Zoezi la uhakiki wa watumishi lawanyima usingizi walimu

Zoezi la uhakiki linaloendelea kwa watumishi wa idara mbalimbali nchini linaloendeshwa na serikali limeacha baadhi ya walimu kukosa usingizi kwani hawana uhakika na ajira zao.

Pamoja na kukosa usingizi kuhusiana na zoezi hilo walimu hao pia wamelalamikia kutoongezewa mishahara na kutopandishwa madaraja kwa wakati huku wengine wakisema kuwa wamekaa kwenye vituo vyao kwa muda mrefu.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kilindi Clemence Mwakasendo amesema kuwa zoezi hilo limeacha pengo kwa walimu kuongezeka na kwa sasa halmashauri hiyo inaupungufu wa walimu zaidi ya mia sita hali iliopelekea kusitisha uhamisho kwa walimu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*