Hali ya uchumi ni mbaya sana – Mhe. Zitto

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo amesema kuwa hali ya kisiasa na kiuchumi ni mbaya sana huku akisema kuwa kwasasa thamani ya shilingi imeshuka.

kizungumza na waandishi wa habari leo, Zitto amesema kuwa mfumuko wa bei umepanda kwa kiasi cha kutisha hasa chakula vyakula na mahitaji muhimu ya wananchi.

“Kama ya uongozi jana imeangalia hali ya kisiasa na kiuchumi kwa ujumla kwa nchi yetu hali ya uchumi ni mbaya sana thamani ya shilingi imeshuka mno, yaani uwezo wa shilingi kununua yani kununua bidhaa umeshuka mno mfumuko wa bei umezidi kupanda mwezi hadi mwezi hasa mfumuko wa bei wa vyakula na mahitaji muhimu ya wananchi, “amesema Zitto.

“Uzalishaji kwenye kilimo umekuwa ukishuka na tumekuwa tukieleza hili kwenye mikutano yetu mbalimbali na waandishi wa habari mikopo kwenye sekta binafsi ukopaji wake umekuwa sifuri kwamba mabenki tena hayatoi mikopo kwa sekta binafsi,” amesema Zitto.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*