Zitto awachana waliojivua uanachama ACT wazalendo

Mbunge wa Kigoma Ujiji ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amewataka wanachama ambao wanaamini chama hicho ni jukwaa la kuitetea serikali, kutoka ACT Wazalendo kwani sio mahali sahihi kwa wao kuwepo.

Zitto Kabwe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishiwa habari katika ofisi za chama zilizopo Kijitonyama jijini Dar es salaam, na kusema kwamba kama watu hao wapo ndani ya chama, ni vyema wakaondoka kama walivyofanya wanachama wengine walioondoka ACT-Wazalendo.

“Tunawaasa wote wanaodhani kuwa chama hichi kitakuwa jukwaa la kuisifia chama tawala na serikali, hili sio jukwaa sahihi kwao, wajitathimini ama kuendelea na uanchama au wajivue kama walivyofanya wenzao”, amesema Zitto Kabwe.

Kauli hiyo ya Zitto Kabwe imekuja siku chache tangu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Samson Mwigamba, kujiunga na chama cha CCM

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*