Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume 2017

Kwa mara ya pili mfurulizo, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa kandada mwaka huu katika tuzo za shirikisho la soka FIFA.

Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid iliyochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania (La Liga )na ligi ya mabingwa Ulaya – (Champions League).

Ninawashukuru sana kwa kunipigia kura, alisema nyota huyo wa Kireno wakati akipokea tuzo yake mjini London. Aliwashukuru mashabiki wake wa Real Madrid, wachezaji wenzake, kocha na rais wake.

Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke aliinyakuwa mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona. Aliwahi pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro 2017.

Facebook Comments