Breaking:Ndege yaanguka hifadhi ya serengeti 10 wanusurika kifo.

Ndege ya Kampuni ya Coastal Aviation iliyobeba watalii 10 imeanguka na kujeruhi watalii wawili na rubani ilipokuwa ikitua katika uwanja wa Lobo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Oktoba 26,2017 Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema amesema ajali hiyo imetokea jana Jumatano Oktoba 25,2017 saa tisa alasiri ilipokuwa ikitua.

Amesema taarifa za awali zinasema chanzo cha ajali hiyo ni mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha iliyosababisha uwanja kujaa maji.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*