Derby ya Kariakoo: Mzani ume-‘balance’

Mambo yamemalizika kwa sare sare katika dimba la taifa baada ya Yanga kufanya mzani wa derby ya Kariakoo uwe sawia (u-balance) baina yao na mahasimu wao Simba SC.

Zilikuwa ni dakika 90 za moto zikiisimamisha Tanzania ‘live’ kupitia Azam Sports 2 kutoka katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam, zilizomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo uliokuwa na ufundi pamoja na mashambulizi ya kila upande, mabao yote yamepatikana kipindi cha pili ambapo Simba ndiyo waliotangulia kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 57 akimalizia kros ya Erasto Nyoni aliyenasa mpira uliopanguliwa na kipa wa Yanga kutokana na shuti la Emmanuel Okwi.

Mara baada ya Kichuya kuitanguliza Simba, Yanga walifanya shambulizi katika kipindi ambacho baadhi ya mabeki wa Simba walionekana kujisahau, na Obrey Chirwa kumalizia kiurahisi pasi ya Geoffrey Mwashiuya kutoka upande wa kushoto, na kufanya mzani u-balance ikiwa ni dakika ya 60 ya mchezo.

Kwa matokeo hayo, Simba na Yanga zimeendelea kuwa na point sawa, zote zikifikisha point 16, lakini Simba ikiwa kileleni kwa idadi kubwa ya mabao.

Facebook Comments