Shiza Kichuya atunukiwa shilingi laki tano kwa kuifunga Yanga

Shiza Ramadhani Kichuya amefunga goli lake la tatu mfululizo dhidi ya Yanga kwenye mechi za Ligi Kuu Bara

Kundi la mashabiki wa Simba, Simba Kwanza limemtunuku kitita cha shilingi 500,000 Shiza Kichuya baada ya mshambuliaji huyo kutajwa kuwa Nyota wa Mchezo kutokana na goli alilowafunga watani wao wa jadi mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Kiwango cha Shiza Kichuya kilikuwa cha hali ya juu hadi kufikia hatua ya kuwashawishi mashabiki hao kumchagua kuwa nyota wa mchezo huo.

Kichuya aliifungia Simba bao la kuongoza lakini baadaye goli hilo lilisawazishwa na Obrey Chirwa na kulazimisha miamba hiyo miwili ya Ligi Kuu Bara kugawana pointi.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo amesema, huo utakuwa ni utaratibu wao wa kila mechi kutoa zawadi ya pesa kwa mchezaji atakaefanya vizuri kwenye mechi.

Ameahidi kuwa, mechi ijayo ya Simba (Mbeya City vs Simba Novemba 5, 2017) watatoa kisasi cha shilingi 2,000,000.

Kelvin Yondani wa Yanga na kiungo mkabaji wa Simba, James Kotei ndiyo waliomaliza mjadala mkubwa wa mechi ya watani kuhusiana na wakali Ibrahim Ajibu na Emmanuel Okwi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*