Mapendekezo mpango wa taifa 2018/19 yakosolewa bungeni

Baadhi ya Wabunge mjini Dodoma wamesema mapendekezo ya mpango wa taifa kwa mwaka 2018 na 2019 hautafanikwa kutokana na sababu mbalimbali mojawapo ni eneo kubwa la mapendekezo hayo kutowagusa wananchi kwa kiasi kikubwa.

Wabunge hao wamesema hayo mjini dododma wakati wakijadili mapendekezo ya mpango wa Taifa kwa mwaka 2018/ 2019 uliwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philipo Mpango bungeni Novemba saba ya mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe katika mipango yote ambayo imewahi kuwasilishwa katika bunge hilo tangu mwaka 2016, halijawahi kuweka kipaumbele kwa wanachi hali ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kwa mipango mapendekezo hayo.

Amesema kuwa mapendekezo hayo hayajagusa eneo la zao la chakula na kuweka bayana kuwa ni ngumu kwa nchi ya Tanzania kutoka katika umaskini kama mapendekezo hayo hayatilia maanani masuala ya chakula.

Suala la kilimo limekuwa na mjadala katika majadiliano ambayo yanaendelea bungeni kuhusu mapendekezo ya mpango wa Taifa wa mwaka 2018 na 2019 huku akisisitiza kuwa wasiporekebisha mapema, huenda wakapata tabu kujinadi katika Uchaguzi wa 2020 na kushauri kuangaliwa vipaumbele vya wananchi na kuachana na mpango wa kufanya kodi ndiyo kipaumbele.

“Hatuwezi kumkamua ng’ombe bila kumlisha, tuangalia wananchi wetu..” Alisema Bashe.

Facebook Comments