Zaidi ya laki 5 kufanya mtihani kidato cha pili

Jumla ya wanafunzi 521,855 wa kidato cha pili ambao wamesajiliwa kufanya mtihani ya upimaji wa wanafunzi wa kidato cha pili wanatarajia kuanza kufanya mitihani hiyo kesho nchini kote.

Akitoa taarifa hiyo, katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dkt. Charles Msonde amesema kuwa mtihani huo utamalizikautaanza Novemba 13 na kumalizika Novemba 24, 2017.

Mbali na mtihani huo, Dkt. Msonde pia amesema wanafunzi wa darasa la nne wanatarajia kufanya mtihani wa kujipima kuanzia Novemba 22 hadi 23 mwaka huu ambapo jumla ya wanafunzi 1,195,970 wamesajiliwa kufanya mtihani huo.

Aidha Dkt. Msonde amesema kuwa mpaka hivi sasa hakuna taarifa za ukiukwaju wa taratibu za mtihani wa kidato cha Nne unaoendelea mpaka hapo majumisho ya pamoja yatakapofanyika.

Facebook Comments