Nassari abadili mtindo wa kufanya kampeni

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemnadi kitofauti mgombea udiwani wa Kata ya Ambureni, Dominick Mollel kwa kugawa CD anazodai zinaonyesha baadhi ya madiwani wa chama hicho wilayani Arumeru walivyoshawishiwa kupokea rushwa

Nassari aligawa zaidi ya nakala 500 katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Kwa Pole wilayani hapa huku akiwataka wananchi kutowachagua wagombea wa CCM kwa kudai baadhi yao wanatuhumiwa kupokea rushwa.

Nassari amefafanua kwamba pamoja na kuwasilisha ushahidi wake Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ameamua kugawa nakala hizo kuwafungua macho wananchi waelewe kwamba wagombea kutoka CCM hawafai.

Akizungumzia kitendo cha baadhi ya wagombea wa CCM kutoa ahadi ya kuyakomboa baadhi ya mashamba yaliyotwaliwa na wawekezaji wilayani humo, Nassari amesema kwamba wakati hao wanatoa ahadi jukwaani wao wataingia shambani kudai haki.

“Wakati wao wanaahidi kushughulika na nyaraka sisi watatukuta shambani tunaendelea na kazi sawa,” alisema Nassari.

Facebook Comments