Tundu Lissu kusafirishwa Ulaya kwa matibabu.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anatarajiwa usafirishwa nje ya nchi kwa matibabu mwezi
mmoja kuanzia sasa.

Familia yake imesema Lissu baada ya kupata matibabu nje ya nchi amepanga kufanya mambo
matano akirejea salama .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 23, kaka wa Tundu Lissu, Wakili Alute Mughwai alisema taratibu za kumsafirisha nje ya nchi zimeanza.

Lissu, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu na mwanasheria mkuu wa chadema amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 alipokuwa akirejea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma Septemba7

“Awamu ya tatu ya matibabu yake ni maalumu sana kwani itahusu pia mazoezi ambayo kama haitafanyika vyema ataweza kupata ulemavu wa kudumu,”alisema.

Hata hivyo, alisema Lissu atapelekwa nje kwa ndege ya kawaida tofauti na hali yake ya awali alipotakiwa kusafirishwa na ndege maalumu za wagonjwa.

“Itatolewa taarifa ni lini ataondoka kwa matibabu na atakwenda nchi gani, hasa baada ya kupata ushauri wa mwisho wa madaktari katika hospitali Nairobi,” alisema.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*