Kibabage aongeza miaka miwili Mtibwa Sugar

Klabu Mtibwaofficial imeongeza mkataba wa Nickson Kibabage kuendelea kutumikia kikosi chake kwa miaka miwili.

Mkataba wa beki huyo aliyefanya vizuri akiwa na kikosi cha Serengeti Boys kilichoshiriki michuano ya AFCON kwa vijana nchini Gabon, ulikuwa ukielekea mwishoni.

Kibabage alijiunga na klabu ya Mtibwa Sugar SC kupitia kituo bora Afrika Mashariki na kati cha kukuza vipaji cha Mtibwa Sugar Academy (under 20) na kabla ya hapo alikuwa anaichezea Moro Kids.

Facebook Comments