BREAKING NEWZZ:Mwenyekiti wa CCM ashikiriwa na TAKUKURU kwa rushwa

ANTHONY Diallo, Mgombea uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, anadaiwa kushikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza akidaiwa kutoa rushwa.

CCM ambacho ni chama tawala kipo katika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali, ambapo kesho Jumamosi utafanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa mkoa wa Mwanza utakaofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba.

Tukio hilo linadaiwa kutokea leo majira ya saba mchana visiwani Ukerewe ambako inaelezwa kuwa Diallo alikwenda visiwani humo kugawa fedha kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi CCM mkoa kumchagua kwa mara nyingine.

Diallo ambaye anachuana vikali na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Meck Sadick baada ya majina ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti katika mkoa huo kutoka amekuwa akitajwa na baadhi ya wanaccm kutembeza fedha kwa wajumbe wa wilaya kadhaa za mkoa huo.

Kamanda wa Takukuru mkoa wa Mwanza, Ernest Makale, alipotafutwa na Mtandao huu, kupitia simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo amesema hana taarifa za tukio hilo huku akidai yupo nje ya mkoa.

Diallo alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi saa 15: 51 (leo) simu yake iliita bila kupokelewa.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*