WANAOISHI NA UKIMWI WAPATA MILIONI 200.

ZAIDI ya Sh milioni 200 zimetolewa na Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) kuyasaidia mabaraza ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi katika halmashauri nane za Kanda ya Mwanza.

Hatua hiyo ni kuziwezesha kuchangia juhudi za serikali kufikia malengo ya taifa.Ofisa Mtendaji Mkuu wa NACOPHA, Deogratius Rutatwa alikuwa akizungumza juzi wakati wa kusaini mikataba ya utoaji wa ruzuku hiyo Nyamagana, Ilemela, Musoma, Kahama, Sengerema, Nzega, Igunga na Muleba.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*