Vyama sita vyaupa kisogo uchaguzi mdogo wa ubunge

Siku 26 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo matatu nchini, vyama sita vya upinzani vimesema havitashiriki kutokana na mazingira ya ushindani kutokuwa sawa gazeti hili kwamba kutokana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokea wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 , vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) navyo havitashiriki.

Wiki iliyopita Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kupitia mkutano uliovihusisha vyama vinavyounda Ukawa; Chadema, NCCRMageuzi, CUF, NLD na Chaumma ambacho kilialikwa, havitashiriki uchaguzi
huo hadi vitakapokutana na NEC na kujadiliana.

Facebook Comments